Ugonjwa wa wasiwasi wa mwingiliano wa kijamii ( Social anxiety disorder) .
Hujulikana kama hofu ya mwingiliano wa kijamii, Ni aina ya ugonjwa wa afya ya akili unaosababisha hofu hasa katika mazingira ya mwingiliano wa kijamii.
Mtu aliye na ugonjwa huu ... hawezi kuchangamana na watu, Hawezi kuzungumza anapokuwa katika kundi la watu, Hawezi kutengeneza urafiki kwa kukutana na watu wapya, Hawezi kuhudhuria mikusanyiko yoyote ya kijamii.
♦️ Dalili za ugonjwa wa wasiwasi wa mwingiliano kijamii....
Mtu aliye na ugonjwa huu unaweza kumsababishia dalili zifuatazo za kimwili kila anapokuwa katika mwingiliano wa kijamii na watu...
〰️Kuona haya usoni, kichefuchefu, kutokwa na jasho, kutetemeka, ugumu wa kuongea, Mapigo ya moyo kwenda kasi, Kizunguzungu, n.k
♦️ Dalili za kisaikolojia za ugonjwa huu zinaweza kujumuisha:
〰️Wasiwasi mkubwa kabla, wakati, na baada ya hali ya mwingiliano na watu.
〰️ Kuepuka hali za mwingiliano na watu katika mikusanyiko yoyote ile.
〰️ Hisia za kuogopa kufanya jambo la aibu hasa unapokuwa katika mwingiliano wa watu wengi.
〰️ Hisia za kunywa pombe au Matumizi yoyote ya madawa ya kulevya kwa ajili ya kukabiliana na mwingiliano wa kijamii..
〰️Hisia kuhusu kujiaibisha au kujidhalilisha.
〰️Hofu ya kuhisi kwamba wengine wanakuona una wasiwasi.
〰️Kuepuka kufanya mambo au kuzungumza na watu kwa kuogopa aibu.
Kila mmoja hupata Wasiwasi wakati fulani, Lakini watu wenye ugonjwa wa Wasiwasi wa mwingiliano wa kijamii wana hofu ya mara kwa Mara katika mwingiliano wao wa kijamii, huhisi kuwa watahukumiwa au watadhalilishwa na watu wengine.
♦️ Watu wenye ugonjwa huu Wanaweza kuepuka hali zote za mwingiliano wa kijamii, ikiwa ni pamoja na:
〰️ Kuuliza swali.
〰️ Mahojiano ya kazi ya kikazi.
〰️ Kutumia vyoo vya umma.
〰️ Kula hadharani.
〰️Kutazamana macho ana kwa ana na watu.
〰️Kuanzisha mazungumzo.
〰️Kuhudhuria sherehe au mikutano yoyoyote ile
♦️ Ni nini husababisha ugonjwa wa wasiwasi wa kijamii?
Ugonjwa wa wasiwasi wa mwingiliano wa kijamii unaweza kutokana na mwingiliano wa sabababu za kibiolojia ( Kurithi au muundo wa ubongo) na sabababu za kimazingira...
♦️ Mambo ya hatari yanayoongeza tatizo la ugonjwa huu...
Sababu kadhaa zinaweza kuongeza hatari ya kuendeleza ugonjwa wa wasiwasi wa mwingiliano wako wa kijamii, ikiwa ni pamoja na:
〰️ Historia ya familia. Kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu ikiwa wazazi wako wa kibiolojia au ndugu zako wana hali hii pia.
〰️ Uzoefu mbaya. watoto wanaopitia dhihaka, uonevu, kukataliwa, fedheha katika malezi yao wanaweza kukabiliwa zaidi na ugonjwa huu. Kwa kuongezea, matukio mengine mabaya maishani, kama vile migogoro ya kifamilia, huzuni unyanyasaji, yanaweza kuhusishwa na ugonjwa huu.
〰️ Mahitaji mapya ya kijamii au kazini. Dalili za ugonjwa wa wasiwasi wa kijamii kwa kawaida huanza katika miaka ya ujana, lakini kukutana na watu wapya, kutoa hotuba hadharani au kufanya uwasilishaji muhimu wa kazi kwa mara ya kwanza kunaweza kusababisha ugonjwa huu kulingana ta tafsiri yako kuhusu uzoefu huo ulioupitia.
〰️ Kuwa na mwonekano au hali inayovutia mwonekano inayovutia umakini kutoka kwa watu.Inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa huu Katika maisha yako ya kila siku.
♦️ Matibabu ya ugonjwa huu...
Onana na Mtaalamu wa afya ya akili ( Mwanasaikolojia na mshauri nasihi) ikiwa una ugonjwa huu kwa ajili ya matibabu ya tatizo lako kupitia Tiba ya Mazungumzo...
Kutafuta msaada wa tatizo lako mapema zaidi kwa kuzungumza na Mtaalamu wa afya ya akili kunaweza kuwa na msaada mkubwa wa kukabilina na tatizo lako au kudhibiti hisia za tatizo lako....
Kuchelewa kushughulikia tatizo lako mapema, Inaweza kuwa vigumu kutibu tatizo lako Ikiwa utaendelea kusubiri..
AHSANTE 🤝...
Nisaidie kushare Makala hii....
TUZIDI KUJIFUNZA, TUSICHOKE KUJIFUNZA ✍️
Kwa Huduma ya msaada wa Kisaikolojia (Tiba ya mazungumzo)..
Pamoja na, Semina au mafunzo ya Elimu ya Afya ya akili ( Magonjwa ya akili), Saikolojia ya Mahusiano, Saikolojia ya Tabia, Saikolojia ya malezi na familia, Saikolojia ya maendeleo binafsi, Elimu ya Stadi za maisha....
Wasiliana nami kupitia namba..
0765900743 { Piga simu....
Imeandaliwa na:-
Psychologist & Counselor,
Author.
Mwlsunzu ✨
№0765900743(WhatsApp