Rubani kipofu anaingia ndani ya ndege, akitumia fimbo yake.
Abiria wote wanatazamana kwa kutoamini.
Kisha mhudumu wa ndege anatangazia abiria na kusema,
"Mabibi na mabwana kama mnavyoona, nahodha ni kipofu, lakini msijali, yeye ni mmoja wa marubani bora zaidi duniani mwenye uzoefu wa zaidi ya saa 6,000 angani".
Kisha, rubani msaidizi nae anapita, pia ni kipofu na anatumia fimbo yake kufika kwenye chumba cha marubani.
Mhudumu wa ndege anatangaza tena,
"Mabibi na mabwana, kama unavyoona, rubani mwenza pia ni kipofu, lakini uwe na uhakika, yeye ndiye rubani wa pili bora zaidi duniani akiwa na zaidi ya masaa 5,000 angani".
Mda mfupi baadae ndege ikaanza kukimbia kwenye barabara yake, kila inapoongezeka kasi, abiria wanatabasamu..
Ndege inaendelea kuongeza kasi zaidi na zaidi hadi ikakaribia mwisho wa njia ya kurukia, bado haijaanza kupaa.
Ndege ikakaribia kabisa mwisho wa njia ya kurukia mara abiria wakaanza kupiga kelele kwa hofu..na ghafla ndege ikaanza kupaa, kisha rubani kipofu anamgeukia rubani mwenza na kusema,
"Siku watakapoacha kupiga kelele ujue tumekwisha"