SOKA LA BONGO| MSIMU HUU HAKUNA VAR



#Bongo SPORTS
TFF YASEMA MSIMU HUU HAKUTAKUWA NA MATUMIZI YA VIKURE (VAR)

Na VENANCE JOHN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limesema msimu huu mfumo wa Video ya kumsadia refa (VIKURE) maarufu kama Video Assistant Referees (VAR) kwa kimombo haitatumika. 

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia ambapo amesema ni mpaka kutakapokuwa na uhakika wa kutosheleza mechi zote kutumia VAR.

Amesema VIKURE ( VAR) inaweza ikatumika katika mashindano yanayojumuisha mechi chache kama vile Ngao ya Jamii.


Post a Comment

Previous Post Next Post