Lugha ya Kiswahili inazungumzwa zaidi katika ukanda Afrika Mashariki ambapo kikanda Eneo hili Lina jumla ya nchi 5 pekee zilizo Mashariki ya Bara la Afrika kiasili,Lakini katika upande wa ncha ya siasa ama kwa engo Jumuiya,Zipo takribani nchi 8 huku Somalia ikijiunga RASMI na jumuiya hiyo mwezi machi mwaka huu.
Lugha Adhwiim ya Kiswahili huchukuliwa zaidi kama kiungo rasmi kwa mawasiliano ya nchi hizi ikifuatiwa na lugha ya Mabeberu ya Kiengereza.Lakini matumizi makubwa ya Lugha ya Kiswahili bado hayajafikiwa kwa kiwango kikubwa kwa nchi zote nane za jumuiya hii kongwe barani Afrika mpaka kufikia kuwa Linguafranka kwa wanajumuiya wote wa Afrika Mashariki.
Taifa la Tanzania ndilo lenye watumiaji Wengi wa lugha ya Kiswahili, Kenya ikifuatiwa kwa ukaribu na Uganda kisha mataifa mengine hufuata yakiongozwa na Rwanda
na Burundi.
Tanzania hujivunia utumiaji sahihi wa lugha hii kwa kukinasibisha na kuwa asili Yake ni kibantu kwa asilimia kubwa huku asilimia chache ni kiarabu Lakini pia bila kusahau kutohoa kutoka lugha za watawala wa kikoloni nchini Tanzania.
GUMZO NA HADITHI YA MTAA.
Baadhi ya watu waishio Tanzania hasa ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki na hata wale baadhi kwa Upande wa Taifa la Kenya na Pwani ya Mombasa hujinasabanisha na Ukweli kuwa Lugha ya Kiswahili ni kiarabu na ndio sababu kuu ya watu wanaoishi pande Za Pwani huongea ama hukitumia Kiswahili katika ufasaha wake.
Je ni kweli Watu wa Tanga na Zanzibar ndio Watumizi wazuri wa Kiswahili kuliko wale walio mbali na maeneo ya Pwani kama Mbeya, Mwanza,na Kigoma.?
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Tanzania,Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi,South Sudan, DR Congo, na Kitinda Mimba.. Somalia.