KWANINI JANA EDGAR KIBWANA AMEMTUKANA SAMATTA?!
--------------------------------
Imeandikwa na Green Osward
Usiku wa jana kipindi cha sports Extra kutoka Clouds FM radio. Kukiwa na watangazaji watatu waandamizi. Shaffih Dauda, Alex Luambano na Edgar Kibwana kontawa. Kuliibuka mjadala wa ghafla kati yao.
Shaffih Dauda aliuliza, kati ya Ibrahim 'Ajibu' na 'Mbwana Samatta,' nani mwenye kipaji halisi cha soka?! Na nani mwenye juhudi bila kipaji?!
Bila aibu wala kuuma maneno 'Edgar Kibwana' akajibu. 'Ajibu' ana kipaji kuliko Samatta. Nilihuzunika sana, ulikuwa usiku wa kuchukiza nisioutamani.
Kilichoniumiza ni kuona aliyejibu hivi ni mtu anayejiita "Doctor wa Seria A."
Mbwana Samatta aliyekuwa mchezaji bora wa Africa ngazi ya klabu. Akiibeba Tp mazembe kwenye mgongo wake. Akaenda ubelgiji akaipa Genk ubingwa wa ligi kuu akiwa mfungaji bora wa timu.
Akacheza EPL na UEFA champions league. Akaifunga Liverpool ya Klop na Mancity ya Guardiola. Tena zikiwa kwenye ubora wa kiwango cha dunia.
"Ajibu" aliyepita Simba, Yanga na costal union, eti ana kipaji kuliko Samatta?! Nahisi kuugua, moyo wangu unavuja damu. Edgar anahitaji kuungama kwa kuidhalilisha miguu ya Samatta.
Ule ni uchambuzi ambao unawakilisha hisia za chuki kwa mafanikio ya Sammata. Ni uchambuzi uliolikosea adabu hata tumbo lililoibeba mimba ya Mbwana.
Aina ya uchambuzi wa aina ile kusikika Radio yenye ukubwa wa Clouds FM. Ni sawa na kuyatia najisi masikio ya msikilizaji anayeufahamu mpira.
Au kabla ya kuingia studio ubongo wa Edgar ulikuwa umezidiwa na maji yanayotengenezwa TBL?! Ulienda wapi utimamu wa fikra za Edgar jana?! Ana ugomvi binafsi na Popa?!
Jana kontawa aliutukana mchezo wa soka hadharani. Ile ilikuwa siku mbaya ambayo ubora wa uchambuzi uligoma kuishi upande wake."
Imeandikwa na Green Osward follow page Yake Facebook.