🚨 #PlayingAbroad : Mtanzania 🇹🇿
MTANZANIA ASHINDA TUZO YA BALLON D’OR HISPANIA
Na VENANCE JOHN
Mtanzania Barka Mpanda, ameandika historia baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya Ballon d’Or kwa watoto chini ya miaka 10 ambayo inaitwa Ballon d’Or of the Champions Dream, huko Hispania.
Tuzo hiyo ilitolewa tarehe 27, 2024, usiku jijini Barcelona na kuashiria mafanikio makubwa kwa nyota huyo aliyepo katika akademi ya CF Damm ya Hispania.
Barka, ambaye ameonesha uwezo wa hali ya juu ndani ya msimu huu, alifanikiwa kuwashinda wachezaji wengine wa kimataifa waliokuwa wakiiwania tuzo hiyo.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Barka alitoa shukrani zake kwa klabu yake, mashabiki wake na familia kwa mchango mkubwa waliotoa katika mafanikio yake.
Katika msimu wake akiwa na CF Damm, Barka ameonyesha umahiri mkubwa, akifunga zaidi ya mabao 10 muhimu na kutoa pasi 8 za mabao ambazo zimepelekea timu yake kuchukua ubingwa wa michuano ya Champions Dream kwa vijana chini ya umri wa miaka 10.
Umahiri wake wa kudhibiti mpira, uchezaji wa kasi, na maarifa kumemfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaotazamwa kama tunu kwenye kikosi hicho.
Tags
Bongo SPORTS.