MAHUSIANO|JE MWANAUME ANAFUATA NINI KWA MWANAMKE

 

MWANAMKE HII NI KWA AJILI YAKO!!!!

 Mwanaume anamfuata mwanamke kwa sababu mbili, NGONO, na MAPENZI, lakini mara nyingi, mwanaume haoi kwenye mapenzi, huoa kwenye UTULIVU.

 Acha nieleze:

 Mwanaume anaweza kukupenda na sio kukuoa.

 Mwanaume anaweza kufanya mapenzi na wewe kwa miaka bila kukuoa.  Lakini mara moja anapopata mtu ambaye humpa utulivu katika maisha yake, anamuoa.

 Ninachomaanisha kwenye Utulivu ni "Amani ya Akili"

 Nimeona baadhi ya wanaume wenzangu wakisema kauli hii

"Nampenda mwanamke huyu lakini sidhani kama naweza kuishi maisha yangu yote pamoja nae."  

Sisi Wanaume ni wenye maono wakati tunapofikiria juu ya ndoa, hatufukirii juu ya nguo za harusi, bi harusi, kitu chochote ambacho wanawake wengi hufikiria kuwa ni fanciful.

Tunafikiria kama mwanamke huyu anaweza kutunza nyumba, Je, anaweza kutunza watoto wangu na mimi pia, Je, anaweza kunipa AMANI ya akili?  

Mwanaume hapendi mwanamke anayempa usumbufu, Ndio maana mwanaume anaweza kukaa na mwanamke kwa miaka mingi na kukutana na mwingine ndani ya mwezi mmoja, kisha kuoana naye.

 Ni faraja kuwa na Amani ya Akili tunayoitaka.

 Mapenzi ni raha, mapenzi ni mapenzi, HESHIMA ni Utulivu

 Biblia inasema "ni afadhali kulala juu ya dari kuliko kukaa na mwanamke mgomvi"

 Ni wazi kwamba maandiko yanazungumza juu ya amani hii ya akili.

 Ngono ni bonasi kwenye uhusiano wa amani katika muktadha wa ndoa. Amani ni muhimu kwa sababu kama ngono pekee ndio inayoweza kumfanya Mwanaume akuoe, basi makahaba wote wangeolewa.

 HITIMISHO

Ninazungumza juu ya maswala ya kweli ambayo yanaathiri uhusiano wa watu.

Post a Comment

Previous Post Next Post