Hadithi:Kwanini ulitumia Jina Langu. ...
Musa alikuwa anaishi Dar es salaam, siku moja aliamua kwenda Arusha kumtembelea rafiki yake Mudi.
Walipokuwa Arusha walipanda gari la Musa na kuelekea Ngorongoro. Lakini wakati wa kurudi usiku, baada ya kuendesha kwa muda mrefu walikwama njiani gari ili haribika.
Hivyo walianza kutafuta msaada wakafika kwenye shamba moja lililokuwa karibu.
Waligonga kwa mwenye nyumba wa shamba hilo, aliyefungua mlango alikuwa ni mwanamke mrembo sana.
Walimuomba kama wangeweza kuwapa sehemu ya kulala usiku huo.
Ninatambua hali mbaya ya hewa huko nje, lakini ninapendelea kuishi peke yangu kwenye nyumba hii kubwa. Hivi karibuni, mwanamke mrembo ambaye mume wangu amefariki alikuja kwangu. Naogopa majirani watanizungumzia vibaya ikiwa nitawaruhusu mkae nyumbani kwangu.
"Usijali," Musa alisema. "Tutafurahi kulala kwenye banda. Na tutaondoka asubuhi sana."
Mwanamke huyo alikubali, na Musa na Mudi hao walielekea bandani kulala humo usiku huo.
Asubuhi ilipofika, walitengeneza gari lao na kuendelea na safari yao. Musa na Mudi walifurahia wikendi nzuri yao huko Arusha.
***
Lakini miezi tisa baadaye, Musa alipata barua isiyotarajiwa kutoka kwa wakili. Ilimchukua dakika chache kuelewa, lakini hatimaye aligundua kwamba ilikuwa kutoka kwa wakili wa yule mjane mrembo aliyekutana naye Arusha alipokuwa na rafiki yake Mudi.
Musa alimfata rafiki yake Mudi na kumuuliza. "Mudi, unamkumbuka yule mjane mwenye sura nzuri mwenye shamba tulilolala kwenye likizo yetu Arusha miezi 9 iliyopita?" "Ndio, nakumbuka." alisema Mudi. "Je, uliamka usiku wa manane, na kwenda nyumbani kwake kumtembelea?" aliuliza Musa. "Ndiyo, nilifanya hivyo." Mudi alisema, kidogo akiwa na haya kwa kubainika.
"Ni kweli nilifanya hivyo."
"Kwa hiyo ulimwambia jina langu badala ya kumwambia jina lako?" Musa aliendelea kumuuliza Mudi.
Uso wa Mudi ulishaanza kubadilika na alijibu.
"Ndio, angalia Musa, kwanza pole rafiki yangu ila unaniogopesha. Kwa nini unauliza hivi?"
Musa alimwambia, "Yule mwanamke amefariki ila ameniacha kila kitu kwa jina langu."
Mwisho