Bondia apoteza Maisha ulingoni.


MSELEMU APITEZA KWA KO,AFARIKI.

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Abbas Mselemu amefariki Dunia baada ya kutandikwa TKO katika pambano la ngumi za kulipwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa habari za mchezo wa ngumi wa Mn boxing Tanzania page inaarifu kuwa Novemba 30, 2024 bondia Mselemu alipanda ulingoni huko visiwani Zanzibar kwenye mapambano ya 'Usiku Wa Left Hook Ya Baba Mwinyi' yaliyo andaliwa na Machatu Boxing Promotion.

Mselemu alicheza pambano la utangulizi la raundi 6 dhidi ya bondia Bakari Bakari mkazi wa huko huko Zanzibar pambano ambalo Mselemu alipigwa na kudondoshwa kwa 'TKO' kwenye raundi ya sita katika mapambano hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Zanzibar Golf Club. 

Baada tukio hilo bondia Mselemu alipoteza fahamu na kupelekwawa hospital ya Mnazi Mmoja ambako huko ndiko alipopatwa na umauti

Mwili wa Mselemu umesafirishwa jana asubuhi na uliwasili jijini Dar es Salaam kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwa taarifa tulizo kuwa nazo bondia huyo alizikwa hiyo hiyo jana  jijini Dar es Salaam.

Tunatoa pole kwa familia ya bondia huyo na kwa wanafamilia wote wa mchezo wa masumbwii kwa msiba huo.

Cc: Munir Boxing Page


Post a Comment

Previous Post Next Post