SANDUKU LA MKEWANGU


Bila D2 huelewi hii story...

Saidi na Fatuma walifunga ndoa.
Wakati wa harusi yao kuisha, Saidi aliona mkewe akiwa na sanduku la chuma lenye ukubwa wa wastani akilificha juu ya kabati lao.

Akiwa na shauku ya kutaka kujua, mkewe alimwambia asiangalie kamwe ndani yake hata iweje.

Miaka mingi ilipita, aliona sanduku hilo la chuma kwenye kabati, lakini kamwe hakuwahi kuchungulia ndani yake kwa ajili ya mke wake.

Siku moja, mkewe alipatwa na kiharusi na kukimbizwa hospitalini.

Saidi akiwa amekaa akihuzunika nyumbani alikumbuka kuhusu sanduku hilo, akalichukua haraka na kwenda hospitalini ambapo mkewe alikuwa amelazwa.

Saidi aliingia kwenye chumba cha mke wake hospitalini na kumsihi amruhusu kulifungua sanduku hilo pembeni yake.

"Sawa," alisema Fatuma, "Nadhani sasa ni wakati sahihi."

Mume alifungua kufuli na kuchungulia ndani.

Upande mmoja akulikuw na midoli miwili iliyosotwa kwa uzi na kwa upande mwingine, kwa mshangao ulikuwa na dola milioni moja.

"Mpenzi, kabla hatujaoana, mama alinipa sanduku hili na kuniambia kuwa kila nikikukasirikia, niende chumbani na kutengeneza mdoli" alisema Fatuma.

Saidi alifurahi na kushukuru. Hakuamini kabisa mke wake alikuwa amemkasirikia mara mbili tu.

"Hii ni ajabu" alisema Saidi kwa mke wake.

"Mpenzi, nashukuru sana kwamba umenikasirikia mara mbili tu, lakini vipi hapa duniani umeweza kupata dola milioni moja?"

"Aah, mpenzi," Fatuma alisema, "Hizo ni pesa nilizopata kwa kuuza midoli mingine ambayo nilisha tengeneza"

Mwisho 😎

Post a Comment

Previous Post Next Post