Makala Fupi.
Ni miaka 7 imeshapita tangu Mudathir Yahya alipotupa maana halisi ya mchezaji wa mkopo! Unakumbuka?
Julai 2017 Mudathir aliomba kutolewa kwa mkopo baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa Mara katika kikosi cha Azam,Kweli wakaridhia ombi lake na akajiunga na Singida United iliyokuwa chini ya kocha Hans Pluijm.
Muda aliwaka haswa mpaka akakabidhiwa kitambaa cha unahodha,Alicheza michezo yote ya #LigiKuu msimu 2017/18,Uwezo aliounesha Mudathir uliwafanya mabosi wa
Azam chap kumpa mkataba mpya wa miaka miwili.
Muda alitoa darasa kwa uchache kwa Wale ambao wanatolewa kwa mkopo,Ukitolewa kwa mkopo ni fursa kuonesha uwezo wako na kupandisha thamani.
Unapotolewa kwa mkopo haina maana kuwa umefeli "HAPANA",unapofunga mlango mmoja mingine mingi inafunguka Amka nenda kapambane!
Tags
Bongo SPORTS.