AFRICA:🟩🟨⬛️WANAOMPATIA LAWAMA ENG. HERSI SAID KWA ISHU YA GAMONDI. HAWAKO SAHIHI.




🟩🟨⬛️WANAOMPATIA LAWAMA ENG. HERSI SAID KWA ISHU YA GAMONDI. NI SAHIHI???

Anaandika Nellove Da Presenter🖋 

Baada ya taarifa ya Young Africans Sports Club kuachana na kocha wake Miguel Gamondi, mashabiki wengi wamepaniki mno huku huzuni zikitawala nyoyo zao mithili ya watu waliopokea taarifa za msiba wa wapendwa wao.

Wapo sahihi...

Maana amewapa mafanikio makubwa mno ndani ya muda mfupi. Achana na ubingwa wa ligi, ubingwa wa CRDB Confederation Cup,  Ubingwa wa Toyota Cup na ngao ya hisani. Achana na vipigo mfululizo kwa mtani Simba SC Tanzania🔴 hususani kile kipigo cha mbwa mwizi (Simba 1-5 Yanga), achilia mbali kuwapeleka wananchi makundi ya CAF Champions League mara ya pili mfululizo pia anayo rekodi ya kuipeleka Yanga SC hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Ni lazima mashabiki wapaniki, ni lazima wahuzunike Ooh!

Ila sasa mashabiki hawajaishia kwenye kupaniki na kuhuzunika tu, wanarusha lawama na golikipa anayetakiwa kudaka lawama hizi ni Rais wa klabu Eng. Hersi Said . Vipi Unadhani wapo sahihi??? Wanampatia lawama Eng Hersi Said kwa ishu ya Gamondi. Ni sahihi???

Kwa upande wangu naona hawapo sahihi japo wao wanahisi wapo sahihi kwani wanaamini, Miguel Gamondi amefungashiwa virago kwa sababu ya matokeo mabovu kwenye mechi mbili zilizopita (Azam & Tabora). Pigia mstari hapo kwenye MECHI MBILI halafu nambie wewe ungeweza??? Nauliza tena wewe ungeweza kumfukuza kocha aliyekupa takribani 85% hadi 90% ya mafanikio ya mipango yako? Unataka kutetea ubingwa kakupa, unataka makundi klabu bingwa kakupa robo fainali,,, kakuongezea hadi Toyota Cup ambayo haikuwa kwenye 'plan' zako. Wewe ungeweza kumfukuza?

Hivi kweli umfukuze kocha kisa mechi mbili wakati karatasi lake la majibu ya mtihani uliompa lina maksi zifuatazo...(Takwimu za Miguel Gamondi tangu atue Yanga SC.)

🏟 — 66 Mechi
✅ — 55 Ushindi
🤝 — 06 Sare
❎ — 05 Vipigo
⚽ — 115 Magoli ya kufunga 
🥅 — 25 Magoli ya kufungwa
🚫 — 42 Clean Sheet
🏆 — 04 Makombe

Najua wewe usingeweza kumfukuza sasa iko hivi, 
Sio wewe tu hakuna mtu yeyote timamu duniani anayeweza kumfukuza kocha mwenye takwimu kama hizo kisa tu kufungwa mechi mbili. HAKUNA.

Hivyo tukijaribu kutumia asilimia 1% tu ya ubongo wetu tunapata kuelewa lazima ipo sababu nyingine nyuma ya pazia iliyomuondoa Mjomba ake Messi pale Yanga. Sasa je hiyo sababu ni ipi????  
Mimi mwenyewe siijui so kama vipi tuendelee kumtupia lawama Injinia Hersi ili wale wanaotumia akili ya kudadavua mambo bila kukurupuka watuone wajinga.

Ni mimi mtu wako wa karibu NELLOVE DA PRESENTER 

Source:NELLOVE DA PRESENT.
#nelloveupdates

Post a Comment

Previous Post Next Post