Ilipoishia
"Ni mchongo gani huo dogo"
Kidika alihoji huku amemkazia macho Yule ambae anamchongo kwa ajili Yake.
Kijana anaingiza mkono mfukoni,tena mfuko wa nyuma kitendo kilichomfanya Kidika apige hatua moja nyuma kujiweka sawa.
La haula kile kilichoonekana....! USO wa Kidika ulibadilika ghafla kwa mshangao mdomo ukimcheza cheza kama mwenye kutaka kutamka jambo...!
SEHEMU YA PILI.
MACHO ya Kidika yalistaajabu kuiona Pete ileile ya Usiku wa Jana,usiku usiosahaulika.Ile hatua moja ya kurudi nyuma ilifanyika kinyume chake sasa alikua mkabala kwa hatua moja kutoka uso wa kijana aliye mbele Yake.
Kidika ni kijana maarufu katika mitaa hii ya Kariakoo ambapo alijizolea jina kubwa na kuwa alwatani juu ya kujihusisha na biashara mbalimbali za watu wengine,yani yeye ni kiungo kiunganishi,dalali...ni dalalili ndio.
Ni kazi anayoipenda kupita chochote kwani ilibadilisha Maisha Yake kwa kiasifulani.Sikumoja miaka kadhaa hapo nyuma alikua amekaa mahali na kuwaza mengi ya maisha yake mpaka pale alipo sasa.
Sauti mbalimbali zilikua zikisikika kichwani mwake,nyingi zilikua zile ambazo hakufurahia kuzisikia.
"Kidika kama hutofuata maamuzi yangu,na Mimi ni Baba yako yatakayo kupata maishani mwako Mungu shahidi"
Sauti ya juu na ukali uliopita kiasi ilisikika ndani ya paa la Mzee Ambumba akimwambia mwanae.
Hili nalo lilibaki kama kumbukumbu kila Mara akilikumbuka,na ilikua akiisikia sauti Ile kwa namna ileile aliyoisikia mwanzoni iliposikika kwenye Ngoma zake.
Kwa wakati huu Kidika anaiangalia Ile pete
akijua fika imeletwa ikafanyike biashara na vichwa vya wanaohitaji.Kwa utaalamu wa muda mrefu alionao aliona kabisa ilikua ni yenye thamani na kwake ni kama "mbuzi kafia kwa muuza supu" Na nikweli Kidika anauwezo wa kumshawishi Mtu yeyote na akatoa kiasi kikubwa kulingana na bidhaa
anayo idalalia.
Wazo la Pete ni wapi aliiona Mara ya mwanzo likaja tena na hapo alisita kuichukua kwanza japo Yule kijana alikua ameiweka mbele Yake biashara mazungumzo iwe lugha ya kweli kati yao.
"UTAPASWA KUKAA KIMYA"
Sauti hii si ngeni masikioni mwa aliyeisikia,ni Dalali Kidika...Mara yamwisho kuisikia ilikua jana... ndipo leo anaposikia sauti hii tena mbele ya Mtu asiyemfahamu,kijana aliye mbele yake.Ni ubongo wake ndio ulitafsiri sauti ile, ni yeye pekee akiisikia.
"Hiyo pete wapi umeitoa"
Swali la MOJA kwa MOJA kutoka kwa mtu wa kati kwenda kwa muuzaji ambaye ni mtu wa upande wa kwanza.
"Unajua blaza nipo kwako tufanye biashara maswali yako siyaelewi,kwani we Huelewi wapi tunapata hizi vitu"
Kijana aliongea kwa msisitizo wa kuchukizwa kiasi huku akiirudisha Pete mfuko wa nyuma.
Kidika aliliona hilo akaona anaenda kuzikosa peza Zipatazo mamilion na mamilion kwa Ile Pete moja tu.Basi alimzuia kisha biashara ikafanyika kila Mmoja alipata alichostahili kwa makubaliano yao wenyewe.
Ile sauti nzito yenye kukwaruza maskio ya msikilizaji ilimkwaa Kidika tena,Mara hii ilimpongeza.
"HONGERA!!"
Ilisema Ile sauti
"Sasa hongera yanini"
Kwa wasiwasi ndani ya korido MOJA ya Gorofa hapo Kariakoo,Kidika aliuliza.
Hakukuwa na kingine zaidi ya jibu la ukimya kumwendea MUULIZAJI.
Baada ya kuona hakuna chamno safari iliendelea kuzipandisha ngazi baada ya kuachana na kordo aliyokuwepo awali,ukomo wa safari ya masafa mafupi kwenda kilele cha jengo lile uliwadia.
Mbele unaonekana mlango ambao Dalali Kidika anaufungua kwa funguo ya aina yake, ni mfano wa waya Lakini uliochongwa kwa alama maalumu kuweka upekee kwa kuzingatia maana ya neno FUNGUO.
Ndani kuna vitu vingi ambavyo viliashiria yeye ni Mtu wa aina gani.
Kulikua na Mali nyingi mno,nyingi, nyingi sana.Alikaa juu ya tivii MOJA kubwa kisha aliwaza kidogo ndipo alipo kumbuka kuwa anamali mfukoni mwake.
Anaitoa na kuiangalia kwa ukaribu zaidi,inaonekana kung'aa sana zaidi ya pale nje,hapa ndani ilikua inawaka kabisa,labda hii ni siri ya Giza.Matamanio ya Pete ile ikae kidoleni ikamjaa...bila hiyana kuiumiza nafsi ili iweje....aliivaa,
Lahaula!!!
Ni kama alifunga macho na kuyafumbua tu hakuamini akionacho, Giza lilitanda mule chumbani na pekee ambacho kiling'aa ni Ile Pete pale kidoleni.Hakuwa na hakika kama kuna uhalisia wowote juu ya mazingira kubadilika na Pete kuwa kidoleni pake.
Maamuzi ya udadisi yalimpeleka mpaka dirishani kufungua nje ...khah!! ni kama usiku tu,tofauti ni kwamba taa hazikuwashwa na shuhuli zilikua zikiendelea pale Kariakoo.
Kidika anafunga madirisha yake na kurudi kwenye tivii Yake kukaa tena.Hofu ilimtanda moyoni na hata nafsini Lakini atafanyaje na ndo maji yameshauona mwili hanabudi kuyapitisha maungoni.
Wazo linamjia Kidika na kuamua kuivua Ile Pete kutoka kidoleni,Waaooh hakuamini hali ilirudi kama awali na bado mng'ao ulikuwa pale pale juu ya lile Giza totoro la awali ndani mle,ni kama awali tu. Giza na mwanga hafifu wa pete vilipendezesha chumba kile.
"Mmmh haya ni Maajabu japo sijaelewa ni kipi kinanikuta hapa"
Ghafla akaivaa tena ili aone Je Giza litarejea?
Ukiomba unapewa watu wa pwani huwa na msemo wao "OMBA UPEWE" Kweli GIZA linarejea na Pete inawaka.Kwa kiasi Fulani ni kama mchezo anaufurahia ,alitabasamu kiasi kisha akataka kuivua tena.
Wapi!!! Pete haikua na mchezo,iligoma katakata.Kila namna imetumika hapa Lakini haikuwa yenye kuleta tofauti kama awali ilivyoanza kwa chomeka chomoa,sasa inamponza Kidika, ghafla...
"Hahahaaaa Hahhhh, Karibu katika ulimwengu wa Giza karibu katika uoni angavu GIZANI"
Sauti yenye mwangwi mkali imemfanya Kidika kuwa wabaridi ilhali mwili unachuja MAJI ya joto Kali,anachemka huku akihisi kuachia haja ndogo.
Ile sauti iliendelea kwa kujirudia mpaka kufikia Mara tatu kisha iliacha na yale maelekezo ya kupewa ukaribisho aliyaona ni ya kweli kwani aliona dhahiri shahiri yumo gizani,Lakini kinacho msaidia ni Ile pete inayoangaza kwa kila apitapo.
Mshangao mkubwa anakutana nao nje alipotoka anaona Maisha yanandelea na watu wakobize wala hawastaajabu mabadiliko ya Giza lililopo pale...
Chaajabu zaidi ni kile anachokiona ...ni kiumbe ,la!! Ni viumbe vipya hakuwahi kuviona,na vyenyewe vipo mihangaikoni kwa wakati ule .......HAKUWAHI KUVIONA
_________________
Je nini kinaendelea,
Maswali ni mengi sana na majibu Yake yapo sehemu ya tatu na zinazo fuata.
USIKOSE.
Andika koment kuhusu Simulizi hii.
Tags
Simulizi za Kitaa.
Mzuri
ReplyDelete