SIMULIZI|SIRI ZA GIZA.



MACHO pekee ndiyo yaliyokua yamefunga, nyakati hizi ni usiku ulitosha kuitwa usiku wa Giza zito, ilikua saa tisa kasoro robo 8:45 mboni za mtu huyu zilionekana zina utelezi mwepesi uliyo jitandaza na kutapakaa eneo lote ambalo hulilinda jicho na 'madhaa' mbalimbali, sijui ni kitugani kimefanya iwe hivyo machoni pake lakini zipo simulizi zinazo elezea hilo kuwa ni mafuta ambayo hujanayo malaika watukufu usiku na kuwapakaa wote walio usingizini kwa wakati huo,huitwa BARAKA...Baraka ya siku mpya.

Mimi sina hakika na hayo zaidi najua ni matongo na kila asubuhi hulazimika kuusafisha usowangu kuyatoa,sasa sijui ndio nazitoa baraka za siku yangu mpya ama la....Keti pazuri Tuianze Hadithi yetu.

Licha ya macho kuwa yapogizani lakini haikutosha kuusitisha Ubongo kufanya majukumu mengi zaidi ya wakati ambao macho huwa yanaangaza kwa ukali maradufu ya GIZA liingiapo,wakati wa Mchana.

Ubongo unachakata, akiwa ndani ya usingizi mzito hofu imemjaa Mtu huyu ambaye pahali alipo lala,godoroni tayari palikua tepetepe, pametepeta jasho lililo mmwagika usiku huu mnene huku sauti za kuneng'eneka kwa anachokipitia usingizini, zilisikika vyema wakati huu huku akivuta pumzi ya nguvu kama anajinasua mahali na tamatiyake alijinasua...anashtuka katika njozi hii ngumu pasipo kujipa nafasi ya kupumua vizuri,haraka anachukua simuyake iliyokua nyuma ya mgongo wake kitandani.

Mboni za yale macho yaliyokua yamefunga mwanzoni wakati huu yanaonekana yakitalii kwenye 'kifaa chake cha mawasiliano' namba iliyokua ikitafutwa punde ilipatikana na simu iliwekwa sikioni Kusikiliza upande wa pili.

"Haloo"
Ule upande ulikua wakwanza kusikika baada ya Muda mfupi.

Mtu huyu ambaye ndiye aliyepiga simu alitoa salamu na kuendelea na mazungumzo yaliyodumu takribani dakika tano.Baada ya hapo mpigaji ndiye aliye kata simu na kuiweka pembeni,ubongo wake haukuchoka kuendelea kupambana kuitafuta suluhu ya kilichotokea muda mfupi kabla ya sasa,ndoto ya kutisha.

Alizama kwenye dimbwi la mawazo ambayo kama ilivyo ada aliwaza mpaka Yale yaliyo nje ya ndoto aliyoiota akijenga hoja kadha wakadha na kuzipigania kutoa majibu Yake yeye mwenyewe.

Mwanaume ambaye wazazi wake walimpa jina la Kidika huku ubini wake ukiwa ni Ambumba.Bwana Kidika Ambumba amezaliwa katika familia ya Wazazi walio na uwezo wa kuyaendesha Maisha yao kutokana na uwezo wa kati na kati walikua nao,Mama alikua ni Daktari katika Hospitali ya Umma na Mzee Ambumba naye ni mwalimu katika shule moja ya serikali iliyo mtaani alipo zaliwa.

Muda ulikwenda sana Kidika alipitiwa na usingizi mwengine pale kitandani,usingizi ambao haukua na mazongezonge kama ya awali hata hivyo sio kama aliufurahia bali kila baada ya Muda mfupi alishtuka Kisa tu ni Ile ndoto aliyoipata usiku wa leo.

Kwani nikitugani ambacho amekiota,tuendelee na hadithi yetu ...

Mwanga wa jua la saa mbili ulipita kwenye paa la nyumba ambamo ndani mwake alikuwemo Kidika akimalizia usingizi wake wa jana,Mara alishtuka na kukaa kitako kabla ya kuchukua maamuzi ya kushuka kwenye godoro lililoko kwenye sakafu.

Muda wote aliokua anajiandaa kupiga mswaki mpaka wakati anaoga alikua akijaribu kuikumbuka Ile ndoto aliyoiota usiku wa asubuhi hii.

Ukomo wa mawazo Yake uliendelea mpaka pale alipofika mahali anapofanyia kazi.

Mwendo mdogo ambao ulikua ukionesha uchovu na dhahiri,hakuridhika na kule kulala 'kimazabemazabe'...

"Boss,Mkuu,Kiongozi,Boss wangu..."
Ni sauti ya kijana Mmoja ambaye aliita Pasi Na kufanikiwa kupata mrejesho wa neno 'NAAM' ...Mwishowe alimfata n kumgusa bega...

"Aaagh Niacheeeee"
Kidika aliguta ukelele uliomshtua Yule aliyemgusa na kufanya aogope kiasi,kumbe ni Kidika ndiye aliyekua anaitwa,ila mawazo we acha tu.!

"Oyaa tunashikana asubuhi asubuhi vipi man..."
Kidika alifoka kistaarabu flani hivi huku akimwangalia aliyembeleyake...mwonekano wake alikua amevaa yeboyebo suruali iliyokatwa magotini na flana imekatwa mabegani,ni kijana mdogo wa makadirio ya miaka kumi na nane hivi kichwani anamfugo mkubwa uliozingira eneo zima.

"Ka'mkubwa usipaniki tulia blaza... ninamchongo hapa, nadhani tuumalize achana na hasira...hizo hazizai mafuba man"
Kijana huyu mdogo aliongea kwa kituo kana kwamba hana uhakika wa anachotaka kukisema kisha akatulia Kusikiliza mrejesho.

"Ni mchongo gani huo dogo"
Kidika alihoji huku amemkazia macho Yule ambae anamchongo kwa ajili Yake.

Kijana anaingiza mkono mfukoni,tena mfuko wa nyuma kitendo kilichomfanya Kidika apige hatua moja nyuma kujiweka sawa.

La haula kile kilichoonekana....! USO wa Kidika ulibadilika ghafla kwa mshangao mdomo ukimcheza cheza kama mwenye kutaka kutamka jambo...!

ITAENDELEA...
Usikose sehemu ijayo pia usisahau Coment yako Muhimu sana kwa muendelezo wa haraka zaidi kujua ni kitugani kimeonekana,ni ndoto gani ameota Kidika na yenye maana gani.





Post a Comment

Previous Post Next Post