Anaandika mdau ✍
TAASISI INAYOONGOZWA NA WATU DHAIFU HAIWEZI KUSIMAMIA MALENGO NA MISIMAMO YA TAASISI
Marehemu baba wa Taifa mwalimu Nyerere aliwahi kusema. Kiongozi mla rushwa hawezi kwenda kumdai Kodi tajiri anayempa rushwa. Kwani yule tajiri atamuuliza hata wewe?
Siku MOJA kabla ya mechi ya Ligi kuu NBC,Dabi ya Dar se salaam kati ya Young Africa na Azam FC Bodi ya ligi ilidharauliwa hadharani na kocha Mkuu wa Yanga Minguel Gamondi.
Katika mkutano na waandishi kuelekea mechi ya Yanga vs Azam kocha huyo alikuja na maji yenye chapa ya GSM bidhaa ambayo si mojawapo inayohitajika kutangazwa katika mkutano ule.
Mwongoza kipindi kiungwana kabisa alimuomba Gamondi kuondoa bidhaa hiyo ila Kwa kiburi Cha hali ya juu alikataa.
Kibaya zaidi mpiga picha mubashara alitumia taaluma yake kujaribu kukwepa kuchukua picha ya Yale maji. Lakini kana kwamba Yale yalikuwa ni maagizo na ilipangwa. Gamondi alilazimisha kuyanyanyua juu Kwa kujifanya anakunywa Yale maji na kuhakikisha nembo inasomeka.
Hiki kiburi kinapatikana wapi?
Au tafsiri yake ni Ile Ile kwamba Bodi ya ligi imetiwa mfukoni na Yanga? Kwamba huyo GSM ana haki ya kufanya chochote na ni kama anawauliza Bodi ya ligi hata nyie?
Kwani amewapa nini Bodi ya ligi mpaka amefikia mahali anajifanyia apendavyo na anawadharau?
Hivi ni kweli Gamondi na Gsm hawajui ni bidhaa gani zinatakiwa kuwepo pale na zipi hazitakiwi kuwepo? Kwa nini hata baada ya kuambiwa aligoma?
Au Kuna makubaliano kama Yale ya kudhamini vilabu kwamba hiyo bidhaa itangazwe Bodi mmeingia kimya kimya na Gamondi anajua ndio maana anakuwa mkali?
HII INAITWA UKIMDEKEZA MBWA ATAKUFUATA MPAKA MSIKITINI.
( Jicho la tatu la Mgalilaya).
@ligikuu @tanfootball @championshiptz @firstleaguetz @nbc_tanzania @azamtvtz
#maskinihachoki
Tags
Bongo SPORTS.