SOKA LA ULAYA|USIKU WA BALLON D'OR MAKALA

Kiungo wa kati wa Man City na Uhispania Rodri ashinda tuzo ya Ballon d'Or kwa wanaume

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAG

Kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa wanaume - tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka - kwa mara ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alipoteza mchezo mmoja pekee msimu uliopita kwa klabu na taifa, alitunukiwa tuzo hiyo mjini Paris baada ya kuisaidia Uhispania kushinda Euro 2024 mwezi Julai.

Pia alishinda Ligi Kuu, Uefa Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia akiwa na City.

Rodri, mchezaji wa kwanza katika historia ya klabu hiyo kushinda Ballon d'Or, alishinda tuzo hiyo mbele ya winga wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr.

Kiungo wa kati wa Real Madrid Jude Bellingham alikuwa wa tatu - akiwa mchezaji wa juu zaidi wa Uingereza aliyemaliza katika tuzo hiyo tangu Frank Lampard kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 2005.

Real Madrid ilishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka na meneja wao Carlo Ancelotti alikuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa wanaume, lakini hakukuwa na yeyote kutoka klabu aliyehudhuria kupokea zawadi hizo.

Iliripotiwa mapema Jumatatu kuwa Real Madrid walikuwa wakisusia sherehe hizo baada ya ripoti kuwa Vinicius hangeshinda Ballon d'Or.

"Ni siku maalum kwangu, familia yangu na nchi yangu," alisema Rodri, ambaye alionekana jukwaani akitembea kwa magongo baada ya kupasuka kwa mishipa yake ya mbele ya mguu (ACL) mwezi Septemba.

"Leo sio ushindi kwangu, ni kwa mpira wa miguu wa Uhispania, kwa wachezaji wengi ambao hawajashinda na wamestahili, kama [Andres] Iniesta, Xavi [Hernandez], Iker [Casillas], Sergio Busquets, wengi sana.. Ni kwa ajili ya soka ya Uhispania na sura ya kiungo cha kati."





  • Emilino Martinez

Rodri alituzwa kwa kuishindia klabu na nchi yake

Tuzo ya Ballon d'Or inamtambua mwanasoka bora wa mwaka na hupigiwa kura na baraza la waandishi wa habari kutoka kila moja ya nchi 100 bora katika viwango vya ubora vya Fifa duniani kwa wanaume.

Ilikuwa ni mara ya kwanza tangu 2003 ambapo hakuna mshindi mara nane Lionel Messi, 37, au mshindi mara tano Cristiano Ronaldo, 39, kuonekana kwenye orodha ya walioteuliwa.

Akiwa ameisaidia Manchester City kutwaa Treble{Mataji Matatu} mwaka 2023, Rodri alimaliza wa tano katika tuzo ya Ballon d'Or mwaka jana.

Mafanikio yake yanayoendelea akiwa na City na nafasi yake ndani ya timu ya Uhispania iliyoshinda Euro 2024 imemfanya kuwa mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa katika soka la dunia.

Mchezaji huyo wa kati alitoka nje akiwa ameumia wakati wa mapumziko katika mechi ya fainali ya Euro dhidi ya Uingereza, lakini alikuwa tayari amefanya ya kutosha kutangazwa mchezaji bora wa michuano hiyo.

Rodri alifunga mabao tisa bora zaidi kwa City msimu uliopita, ikijumuisha magoli mawili muhimu ya dakika za mwisho katika mechi za Ligi Kuu ya Uingereza na bao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham.

“Leo marafiki wengi wameniandikia na kuniambia kuwa soka imeshinda, kwa kuwapa nafasi viungo wengi wa kati ambao wana kazi nyingi na leo inadhihirika,” aliongeza Rodri ambaye alikabidhiwa tuzo hiyo mwaka na mshindi wa mwaka 1995 George Weah.

"Mimi ni mvulana wa kawaida mwenye maadili, ambaye anasoma, ambaye anajaribu kufanya mambo sawa , na nimeweza kufika kileleni na ni shukrani kwenu nyote. "

Alipoulizwa kuhusu jeraha la ACL ambalo litamfanya awe nje kwa msimu huu, alisema: "Ninajaribu tu kujitunza, kupumzika, kufurahia wakati wa mapumziko na familia yangu na nirudi nikiwa na nguvu zaidi."

Kane na Mbappe walishinda tuzo ya Gerd Muller

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Harry Kane

Harry Kane na Kylian Mbappe walishiriki Tuzo ya Gerd Muller - tuzo ya mfungaji bora - baada ya wote kufunga mabao 52 katika mashindano yote msimu uliopita.

Huku fowadi wa Real Madrid na Ufaransa Mbappe akiwa hayupo, nahodha wa Uingereza Kane alikabidhiwa tuzo hiyo peke yake kufuatia msimu mzuri wa kwanza akiwa na Bayern Munich.

"Asante kwa klabu yangu ya Bayern Munich, wafanyakazi wangu wote, wachezaji wenzangu, kwa kunisaidia kufunga mabao yote niliyofunga," alisema Kane, ambaye alimaliza katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa tuzo ya Ballon d'Or kwa wanaume.

"Ni heshima kuchukua tuzo hii kutoka kwa gwiji wa klabu [Karl-Heinz Rummenigge] - asante sana."

Real Madrid yashinda tuzo za klabu na kocha bora licha ya kususia hafla hiyo

Wakati Real Madrid ilishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka na Ancelotti akapata Tuzo ya kwanza ya Johan Cruyff ya kocha bora, hakukuwa na hotuba.

Badala yake sherehe iliendelea kwa kasi.

Chini ya Ancelotti, Real Madrid walishinda La Liga kwa pointi 10 msimu uliopita pamoja na Kombe la Super Cup la Uhispania, huku pia wakitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa - wakishinda taji lao la 15 katika mashindano hayo.

Walikuwa na wachezaji saba walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or kwa wanaume.

Yamal ashinda tuzo ya Kopa

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lamin Yamal

Tuzo ya Kopa Trophy, iliyotolewa kwa mchezaji aliyefanya vizuri zaidi chini ya umri wa miaka 21, ilienda kwa winga wa Barcelona na Uhispania Lamine Yamal.

Yamal, ambaye alitimiza umri wa miaka 17 mwezi Julai, aliichezea Barcelona mechi 50 msimu uliopita, akifunga mabao saba na asisti saba.

Alikuwa sehemu ya timu ya Uhispania iliyoshinda Euro 2024 ambapo pasi zake nne za mabao nchini Ujerumani zililingana na rekodi ya mchezaji yeyote katika michuano ya Ulaya.

Akiwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi, mfungaji mabao na mshindi kwenye Euro, Yamal alitajwa kuwa mchezaji mchanga wa mashindano hayo.

Martinez ashinda tuzo ya pili ya Yashin mfululizo

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Emiliano Martinez aliichezea Aston Villa mechi nane bila kufungwa msimu uliopita

Mlinda lango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez alishinda taji la Yashin Trophy - tuzo ya golikipa bora - kwa mwaka wa pili mfululizo.

Martinez, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka wa 2022, aliisaidia Aston Villa kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi ya Premia msimu uliopita na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 pia alichangia pakubwa kwa Argentina kushinda Copa America na kutofungwa hata bao moja katika michezo mitano kati ya sita..

"Kushinda mara moja ni heshima, kushinda mara ya pili mfululizo ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia," alisema Martinez, ambaye ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya golikipa bora mara mbili mfululizo.

Washindi 10 bora wa tuzo ya Ballon d'Or

  • Rodri (Spain and Manchester City)
  • Vinicius Jr (Brazil and Real Madrid)
  • Jude Bellingham (England and Real Madrid)
  • Dani Carvajal (Spain and Real Madrid)
  • Erling Haaland (Norway and Manchester City)
  • Kylian Mbappe (France and PSG/Real Madrid)
  • Lautaro Martinez (Argentina and Inter Milan)
  • Lamine Yamal (Spain and Barcelona)
  • Toni Kroos (Germany and Real Madrid)
  • Harry Kane (England and Bayern Munich)
  • Source BBC SWAHILI.

Post a Comment

Previous Post Next Post